
Kiongozi wa idara ya wakimbizi nchini Uganda amekana madai kwamba Kampala inapanga kuwafurusha wakimbizi wa Burundi waliopo nchini humo kufuatia agizo la serikali ya Burundi.
Kamishna wa wakimbizi David Apollo Kazungu amesema kuwa
serikali itaendelea kutoa hifadhi kwa wakimbizi wa Burundi hadi wakati ambapo
itakuwa salama kwa wao kurudi nyumbani.
Chombo cha habari cha Duetsche Well kiliripoti kwamba Uganda
ilipanga kuwarudisha nyumbani kwa lazima wakimbizi 46,000 kutoka Burundi
kufuatia ombi la serikali yao.
DW ilisema kuwa waziri wa wakimbizi nchini Uganda Hillary
Onek alinukuliwa akisema: Mumepewa Visa ya kuishi kwa miezi mitatu na iwapo
Visa yako inaisha hatutafanya kama alivyofanya Trump bali tutawashauri warudi
nyumbani polepole.
Burundi imekabiliwa na ghasia tangu rais Pierre Nkurunziza
kuamua kuwania urais kwa muhula wa tatu mnamo mwezi Aprili 2015.
Mamia ya watu wamefariki tangu ghasia hizo kuanza huku takriban raia 240,000 wakitorokea Tanzania, Rwanda, DR Congo na Uganda.
No comments:
Post a Comment