
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam, limemtaka
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kujisalimisha Polisi
mara moja kwa ajili ya Mahojiano yanayohusu vita vya dawa za kulevya baada ya
juhudi za kumsaka katika makazi yake kushindikana huku simu yake ya mkononi
ikiwa imezimwa
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Simon Sirro amesema Bw. Mbowe aliahidi kwenda
mwenyewe juzi tarehe 15, lakini hakwenda lakini jeshi la hilo lilimtafuta usiku
na mchana katika makazi yake na kumpigia simu lakini simu yake ilizimwa
Aidha jeshi hilo limesema watuhumiwa watatu Agnes Masogange,
Rashid Idd au Chid Mapenzi na Wallis Latif Nasher ambaye ni muuza magari katika
eneo la mikocheni watapandishwa kizimbani Jumatatu kwa kosa la kukutwa na dawa
za kulevya lakini pia walibainika wanaotumia dawa hizo baada ya kupelekwa kwa
Mkemia Mkuu
Katika kupambana na Askari feki, jeshi limemtia mbaroni
aliyekuwa askari Magereza wa cheo cha Koplo Peter Elias Msigwa aliyekuwa
mtumishi katika gereza la keko, ambaye alifukuzwa kazi Desemba mwaka jana,
lakini alikamatwa jana akiwa na mavazi ya kiaskari tena akiwa amejipandisha
cheo kutoka koplo hadi Sajenti wa Polisi
Jeshi hilo pia limesema limewatia mbaroni watu 65 kwa kosa
la kukutwa na dawa za kulevya pamoja na watuhumiwa 73 wa wizi na ujambazi wa
kutumia silaha, mitambo mitano ya Gongo, lita 270 pamoja na Puli 250 za bangi.
No comments:
Post a Comment