
Mchekeshaji maarufu kutoka nchini Kenya, Erick Omondi ijumaa
iliyopita ya tarehe 10 alifunguka jinsi Diamond alivyomsaidia kupenya kwenye
soko la Tanzania.
Omondi anasema kwa mara ya kwanza alikutana na Diamond
Mombasa nchini Kenya akiwa kwenye harakati za kurekodi wimbo wa Diamond
unaoitwa Nabeba Mawe.
Katika mazungumzo yao Diamond alimualika Omondi kwenye show
kubwa maarufu kama "Zari All White Part" na kumuomba awe MC wa show.
Katika show hiyo ambayo ilikuwa na zaidi ya wahudhuriaji
10,000 , redio na TV nyingi za Tanzania Omondi hakufanya kosa kama MC, alitumia
kudhihirisha kipaji chake cha uchekeshaji na ikawa ndio mwanzo wa kujulikana
Tanzania.
Omondi anasema bila Diamond kumwalika Tanzania huenda
asingeweza kupenya katika soko la Tanzania, soko lenye mashabiki wengi sana wa
kazi zake.
Mpaka sasa Erick Omondi ana mpango katika kipindi cha miezi
miwili ijayo, kuanzisha Comedy TV show nchini Tanzania kwenye moja ya Runinga
maarufu hapa nchini.
Japo hakuweka wazi kipindi hicho kitarushwa hewani kupitia
kituo cha habari cha shirika lipi.
No comments:
Post a Comment