
WAZIRI Mkuu,
Kassim Majaliwa amepiga marufuku matumizi ya viberiti, mishumaa na hita za
kuchemshia maji kwa wanafunzi wa bweni ili kuepusha majanga ya moto na
atakayekutwa, atachukuliwa hatua kali.
“Kuna tabia
ya baadhi ya wanafunzi hasa wa masomo ya fizikia kutengeneza vifaa vya kienyeji
vya kuchemsha maji mabwenini, jambo hili ni la hatari kwani linaweza
kusababisha ajali ya moto, hivyo ni marukufu kwa mwanafunzi kutumia vifaa
hivyo,” alisema.
Waziri Mkuu
alitoa agizo hilo jana katika harambee ya kuchangisha fedha za ujenzi wa
majengo ya Shule ya Sekondari Lindi, yaliyoungua moto usiku wa kuamkia Julai
10, mwaka huu.
Katika ajali
hiyo shule imeathirika kwa asilimia 34 baada ya vyumba tisa vya madarasa, jengo
lenye matundu 26 ya vyoo na jengo la maabara ya kemia na fizikia yameungua na
kusababishia hasara ya Sh milioni 682.78.
KAMA BADO HAUJAONA HII HAPA HUKO INDIA WANAUME WATAMBIANA KWA KUKATA MAUNO,
KAMA BADO HAUJAONA HII HAPA HUKO INDIA WANAUME WATAMBIANA KWA KUKATA MAUNO,
VIDEO :
No comments:
Post a Comment