
Marekani
imeitaka Uturuki kujizuia baada ya jaribio la mapinduzi lililozimwa siku ya
Ijumaa ambapo maelfu ya maafisa wa kijeshi wamekamatwa.
Waziri wa
mashauri ya nchi za kigeni nchini Marekani John Kerry ameutaka utawala nchini
Uturuki kuheshimu sheria wakati wa uchunguzi wao kuhusu mapinduzi hayo.
Kerry
amesema kuwa madai kwamba Marekani ilihusika katika mapinduzi hayo inasababisha
madhara kwa uhusiano kati ya washirika hao wawili wa NATO.
Mapema kupitia kwa hotuba yake, rais wa
Uturuki Recep Tayyip Erdogan alitoa wito kwa rais Obama kumrejesha nchini humo
kiongozi wa kidini raia wa Uturukli anayeishi nchini humo Fethullah Gulen
ambaye analaumiwa kwa kupanga mapinduzi hayo.
JE ULIMISS VIDEO TAMU YA WHATSAP VITUKO?? HII HAPA MTU WANGU BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA!
No comments:
Post a Comment