
Kwa mujibu
wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Katibu Mtendaji wa BASATA,
Godfrey Mngereza ameeleza kuwa msanii huyo amekuwa na tabia na mienendo yenye
kuchafua sekta ya sanaa yeye binafsi kupitia kutoa kazi chafu na kufanya
maonyesho yenye kukiuka maadili.
“Kazi zake
zikikiuka maadili na kudhalilisha utu wa mwanamke sambamba na kutoa lugha za
matusi na za kudhalilisha watu wa kada mbalimbali.” alisema Mngereza.
Aliongeza,
“Ikumbukwe kwamba BASATA limeshamuita na kumuonya msanii huyu mara kadhaa
kutokana na tabia yake ya kutoa kazi zisizokuwa na maadili na aliahidi
kubadilika na kuachana na tabia hiyo. Kwa hiyo kuendelea kwake kufanya matukio
haya kwa makusudi ni uthibitisho kwamba hajabadilika na kwa maana hiyo
ameendelea kuidhalilisha sanaa na wasanii wa kitanzania wenye kujitambua na
kuiheshimu kazi ya sanaa kama kazi nyingine. Kwa sasa Msanii huyu ametoa wimbo
mwingine wa ambao uko mitandaoni ukipambwa na picha chafu zinazoonesha mwanamke
akiwa mtupu yaani uchi wa mnyama.”
No comments:
Post a Comment