
WAKATI baadhi ya mabinti wanaohusika
kama video queens kutajwa katika sakata la madawa ya kulevya hivi karibuni,
Gift Stanford ‘Gigy Money’ ameibuka na kusema baadhi yao wanaponzwa na kuiga
aina ya maisha anayoishi, hivyo kujikuta wakijihusisha na ishu hiyo.
“Naona wanapenda kuniiga maisha
yangu sana, sijawahi kubeba au kutumia unga na sina hofu kabisa ya kutajwa
maana huwa nafanya kazi halali, hao video queen wanaoiga na kutaka kuwa juu
kama mimi hawajui kwamba siri ya mafanikio yangu ni kufanya kazi,” alisema
msanii huyo ambaye licha ya kuwa video queen, pia ni mtangazaji wa redio.
Katika vita alivyoanzisha vya
kupambana na madawa ya kulevya, Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda alitaja
majina ya watu mbalimbali wanaotuhumiwa kujihusisha nayo, wakiwemo video
queens, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’ na Tunda Sebastian ambao walifikishwa katika
Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu na kuachiwa kwa dhamana.
No comments:
Post a Comment