Bwana harusi na bibi harusi wazirai kanisani muda mchache kabla ya ndoa yao - boazmwakasege.com

MADA MOTO

Wednesday, December 14, 2016

Bwana harusi na bibi harusi wazirai kanisani muda mchache kabla ya ndoa yao

 Huko Kilimanjaro wilaya Moshi kuna moja kati ya matukio ya nadra kuwahi kutokea katika familia, baba mzazi wa mmoja wa maharusi mwishoni mwa wiki aliibuka kanisani saa chache kabla ya muda uliopangwa kufunga harusi, na kuweka pingamizi. Maharusi waliopatwa na mkasa huo ni Yohana Mohammed na Rose Sembeye.

Kitendo cha mzazi wa Yohana kuweka pingamizi kilisababisha maharusi wote wawili kupoteza fahamu, na licha ya harusi kutofungwa, wawili hao waliamua kwenda ukumbini kuungana na waalikwa saa 11:00 jioni wakitokea hospitalini ambako walikuwa wamepumzishwa.
Source: Mwananchi

No comments:

Post a Comment