
Msanii Baraka The Prince amezungumzia sakata la mpenzi wake Najma na Mr.
Blue ambaye alikuwa mpenzi wake, na kusema tukio hilo halikuwa na
ukweli wowote na hata kama lingekuwepo, hawezi kuzuia wawili hao
kuwasiliana.
Akizungumza kwenye kipindi cha Bongo Fleva Top 20 cha East Africa Radio,
Baraka amesema yeye hawezi kuzuia wawili hao kuwasiliana kwani wote ni
wasanii, na pia hana kawaida ya kushika simu ya mpenzi wake na kujua
amewasiliana na nani.
“Hamna zile stori sio za kweli, hata mimi Blue alivyoniface nilimwambia
sijui hizo habari na sijawahi kuona ukimpigia, hata ukimpigia we ni
mwanamuziki mwenzake, mi siwezi nikamuwekea mipaka Najma, au eti siwezi
kuwekea mipaka hey Bro usimpigie Najma, kwanza mi hata kugusa tu simu ya
Najma sijawahi na hata Najma kugusa simu yangu hagusi yangu, haijawahi
kutokea tu kitu kama hicho sasa sijui kilitokea wapi”, alisema Baraka
the Prince.
Baraka aliendelea kusema ingawa tukio hilo liliathiri kwa upande
mwingine, lakini alijaribu kukaa na Mr. Blue kumshauri kuyapuuzia
masuala hayo, na amtulize mkewe asisikilize ya watu.
“Mi nilimuelewa Blue kwa sababu Blue alikuwa analalamika kweli kwamba
mwanamke wake anammind, kwenye familia yake hamna amani, mi niliheshimu
kwa sababu najua haya mambo yalivyo, lakini mi nilijaribu kuongea naye
nikamwambia amwambie shemeji atulie sio kweli bwana”, alisema Baraka the
Prince.
No comments:
Post a Comment