
Baada ya taarifa za mfanyabiashara na mwenyekiti wa
klabu ya Dar es Salaam Young Africans Yusuph Manji kuripotiwa kukusudia
kujiuzulu wadhifa wake huo ndani ya klabu ya Yanga kwa kile kinachodaiwa kuwa
ni kuandamwa na maneno na baadhi ya watu huku wana Yanga wengine wakiwa kimya.
Taarifa za
Manji kujitoa zinakuja kwa sababu ya kudaiwa kujihisi mpweke kwani licha ya
kushambuliwa kwa maneno na baadhi ya ya watu ikiwemo wanasiasa, hakuna
mwanayanga aliyekuwa pamoja nae hivyo anajihisi mpweke na ana kusudia kujiweka
pembeni.
Kufuatia
taarifa za Manji kukusudia kujitoa viongozi wa Yanga wa kanda zote wamekusudia
kufanya kikao leo saa 4 asubuhi makao makuu ya klabu hiyo kutoa tamko la pamoja
kuhusiana maamuzi ya Manji, kujitoa kwa kuona anatengwa na wanachama.
No comments:
Post a Comment