Jeshi la
polisi mkoa wa Njombe limekamata silaha moja ya kivita na risasi 122
zilizokutwa na watuhumiwa nane wakiwa na silaha nyingine za jadi walizo tumia
kufanya uhalifu katika maeneo mbalimbali ya mikoa ya Njombe na Iringa.
Kamanda wa
polisi mkoa wa Njombe Pudensiana Protas akizungumza na waandishi wa habari
amesema kuwa watuhumia hao walikutwa na silaha ya kivita yenye darubini aina ya
long riffle, huku akizitaja silaha za jadi kuwa ni pamoja na shoka na nondo
zinazodaiwa kuhusika katika matukio mbalimbali ya wizi.
Silaha ya
aina hiyo inakamatwa ikiwa ni mara ya pili tangu kuanza kwa mwaka huu ambapo
silaha zote zimekamatwa wilaya ya kipolisi Makambako na watuhumiwa watafikishwa
mahakamani uchunguzi wa jeshi hilo utakapo kamilika.
Aidha
inadaiwa watuhumiwa hao walikutwa na dawa ya meno pamoja na mafuta ya kupaka.
CHANZO: MTEMBEZI.COM
No comments:
Post a Comment