
Mbunge wa
Chalinze Mhe. Ridhawani Kikwete amewapongeza wasanii wa muziki, Diamond
Platnumz na AliKiba kwa kutoa msaada wa tsh 41milioni kwa ‘GSM Foundation’ ili
kusaidia jitihada za taasisi hiyo za upasuaji wa watoto wenye vichwa vikubwa na
mgongo wazi.
Diamond na
Ali Kiba
Mtoto huyo
wa Rais mtaafu, amewapongeza wasanii hao kwa kuonyesha kuguswa na kusaidia
matatizo ambayo yanatokea katika jamii.
“Katika vitu
vimeonyesha umuhimu wa kuwa stars katika jamii yetu ni hili mlilolifanya wadogo
zangu. Ni jambo la kusifiwa na Mungu atawalipa kwa kuwaongezea maarifa ya
kufanya kazi zenu vizuri,” Ridhiwani aliandika katika instagram yake.
Aliongeza,
“Pia niwapongeze sana GSM Foundation kwa kazi nzuri mnayoifanya. Kutoa si
utajiri, ni moyo na mungu atakuzidishia ndugu mkurugenzi Gharib pale ulipotoa.
Kila la kheri katika kusaidia jamii yetu yenye mahitaji. Peace to you,”
Siku chache
zilizopita Diamond Platnumz alitoa msaada kwa taasisi hiyo wa tsh 20 Milioni na
baadae AliKiba na yeye aliamua kutoa tsh 21 Milioni.
No comments:
Post a Comment