Inakadiriwa
kuwa mali zenye thamani ya mamilioni ya shilingi ya Kenya zimeharibiwa na moto
huo, huku mamia ya wanafunzi wakikosa mahala pa kulala.
Mabweni ndio
yaliyochomwa moto hali iliyosababisha wanafunzi kupoteza mali zao kama vile
vitabu na nguo zao ikiwemo za shule.
>>>Matukio ya
shule kuungua moto yamekuwa yakiongezeka katika siku za hivi karibuni nchini
humo.
Mapema wiki
hii wanafunzi 42 walipandishwa kizimbani nchini Kenya, katika mahakama tofauti
kwa tuhuma za kuhusika na uchomaji moto shule.
Wengi wao
wameachiwa kwa dhamana huku wakifanyiwa uchunguzi wa umri kuona ni nani ana
umri wa kuweza kushtakiwa kama mtu mzima ama kushtakiwa kama mtoto.
Serikali ya
Kenya imesema itawachukulia hatua kali wale wote watakao bainika kuhusika na
matukio hayo.
Chanzo: BBC news
Chanzo: BBC news
KAMA BADO HUJAPITIA KURASA ZA MAGAZETI YA LEO KATIKA UDAKU, HARDNEWS, NA MICHEZO, BASI NIMEKUSOGEZEA MTU WANGU, SOMA HAPA
No comments:
Post a Comment