Msanii wa
filamu na muziki, Baby Madaha amekanusha taarifa ambazo zilizagaa katika
mitandao ya kijamii kuwa amefunga ndoa na mwarabu wa Dubai.
Mapema mwaka
huu gazeti moja kubwa liliripoti taarifa ya kuwa msanii huyo wa filamu alifunga
ndoa kimya kimya na mwarabu wa Dubai baada ya ukukubali kubadii dini na kuwa
muislam.
Akiongea na
Bongo5 Jumanne hii, Baby Madaha alisema kilichofanyika wakati huo ambacho
kinadaiwa ilikuwa ni ndoa, ulikuwa ni utambulisho wa mpenzi wake huyo kwa
wazazi wake.
“Ndoa bado
sijafunga kama baadhi ya watu walivyosema ila nimeveshwa pete ya uchumba na
nimemtambulisha mpenzi wangu kwa wazazi” alisema Baby Madaha.
“Kusema
kweli kila kitu kinaenda sawa na tayari nimeshavalishwa pete ya uchumba, sema
sikutaka kutangaza kwa sababu wasanii wengi wamekuwa wakiishia katika pete za
uchumba, kwa hiyo niliona nikishafunga ndoa ndio nitaweka wazi,” aliongeza.
Pia
mwigizaji huyo amesema amekubali kubadili dini na kufunga ndoa ya kiislam.
“Unajua sisi
wasichana, watu wanasema hatuna dini, kwa hiyo mimi binafsi kama mama yangu
akiwa tayari nitafunga ndoa ya kiislam kwa sababu haya ni maisha,” alisema Baby
Madaha.
No comments:
Post a Comment