
WAUZA nyago
kwenye video za Kibongo, Lulu Abass ‘Lulu Diva’ na Gift Stanford ‘Gigy Money’
hivi karibuni wamechimbana mikwara na kupakana shombo kila mmoja akimuona
mwenzake kituko kutokana na maneno anayoyasikia juu yake.
Ishu nzima
ilianza baada ya mwandishi wetu kupata ubuyu kutoka kwa mmoja wa watu wa karibu
wa Lulu Diva kuwa anamhofia Gigy Money kumfunika katika gemu wanalofanya.

Baada ya
mwandishi wetu kupewa ubuyu huo alimwendea hewani Lulu, aliposomewa madai hayo mwanadada huyo alisema;
“Nani
kakwambia hivyo? Siwezi kumhofia Gigy kwenye kile ninachokifanya, hana kitu
chochote cha kunifanya nimhofie maana ni mtu wa kawaida sana kwangu.”
Kwa upande
wa Gigy alipotafutwa alisema; “Siwezi kupigizana kelele na huyo demu, anatafuta
kiki kupitia kwangu lakini hawezi kuipata hata kwa dawa, haniwezi kwa kila
kitu, akajipange sana na akae akijua simuogopi.”
No comments:
Post a Comment