Baada ya
kuenea kwa habari za mshambuliaji wa kimataifa wa Ivory Coast anayeichezea
klabu ya Azam FC Kipre Tchetche kuripotiwa kusaini klabu ya Nahda Al-Buraimi ya
Oman, afisa mtendaji mkuu wa klabu hiyo Saad Kawemba ameeleza ukweli na kuwatoa
hofu mashabiki walioshtushwa na habari hizo.
C.E.O wa
Azam FC Saad Kawemba kaeleza kuwa hizo ni habari za uzushi za kuwa nyota wao
amesaini Nahda Al-Buraimi ya Oman, kwani bado ana mkataba na Azam FC ndio maana
hata vyombo vya habari vinaripoti kuwa anaomba akapate changamoto mpya kwa
maana ana mkataba na Azam FC.
“Kipre ni
mchezaji wetu ambae ni muhimu huwezi kumruhusu amalize msimu aende mapumziko
akiwa hana mkataba, kwa hiyo tuna mkataba ambao ni endelevu, nadhani ndio maana
ukasikia wanasema anaomba akapate changamoto sehemu nyingine, ukweli ni kuwa
mchezaji kama ana mkataba ni makubaliano umuuze au anunue mkataba”
No comments:
Post a Comment