Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani imesema hakuna polisi yeyote wa
kikosi hicho anayelipwa bonasi kutokana na ukamataji na ulipaji wa faini
zinazotokana na makosa ya usalama barabarani.
Taarifa zinazosambaa kwa watu mbalimbali na katika mitandao ya kijamii,
zinadai kuwa trafiki kwa kila kosa analokamata na kutoza faini katika
kila sh 30,000, analipwa Sh 5,000 kama bonasi.
➤ MAJAMBAZI Yapora Mamilioni Mbele ya Askari polisi Dar -
Ufafanuzi juu ya suala hilo ulitolewa Jumatano hii na Kamanda wa Kikosi
cha Usalama Barabarani, Mohammed Mpinga wakati akizungumza na Habarileo
ofisini kwake. Alisema hakuna ukweli kwamba askari hao wanapata asilimia
fulani kutokana na makosa wanayokamata, bali wamepewa maelekezo ya
kukamata makosa mengi kadri wanavyoweza.
“Nafikiri hii inatokana na kukamata makosa mengi, lakini niseme hakuna
askari anayelipwa bonasi, wanachokifanya ni kukamata kulingana na makosa
tu,” alisema Kamanda Mpinga.
➤ ASKARI wa wanyama pori mbaroni kwa kuua na kuficha maiti.
➤ HATIMAYE Aliyechomwa Mkuki Mdomoni Arejea Nyumbani.
Aidha, alisema zipo taarifa kuwa askari hao wamepangiwa idadi ya makosa,
jambo alisema si kweli ila wamepewa maelekezo ya kukamata makosa mengi
kadri inavyowezekana, ikiwa ni kwa lengo la kudhibiti ajali.
Friday, January 6, 2017
Kamanda Mpinga Akanusha Trafiki Kulipwa Bonasi Kwa Kukamata Magari
Tags
# HABARI
Tupe Maoni Yako (Matusi Hapana)
Mwakasege Blog
USIACHE KU LIKE PAGE YETU KWAKUBONYEZA LIKE BUTTON
About siasa
HABARI
Labels:
HABARI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
Mahala popote ulipo, unaweza kututumia Habari kupitia namba yetu ya whatsap +255756584473.
No comments:
Post a Comment